Mapendo ya mama yashinda yote.

 

Synopsis

Miili ambayo imefanywa kua uwanja wa vita sio tu ina makovu ya ubakaji. Mara nyingi pia huzaa watoto. Akina mama na familia zao wamekua wahanga wa stigmatization katika jamii ijapo kua ni jamii hiyo ingalipashwa kuwafariji na kuwasaidia. Katika filamu hii, "Letter to my child from rape", filmmaker Bernadette Vivuya analeta kwenye skrini maneno yenye nguvu yake poet na mwanasheria Désanges Kabuo
Huyu ameshinda ubaguzi na anadai kesho bora na ya matumaini kwa mtoto wake ambaye hakuchagua kumzaa, lakini ambaye kwa sasa anapenda sana na kujivunia.

Timu

 

Directed and Produced by Bernadette VIVUYA

Bernadette Vivuya ni mwandishi wa habari na mtengenezaji wa filamu anayeishi pa Goma, mashariki mwa DRC. Amejifunza Social justice photography: Decomposing the colonial gaze kwenye center Yole!Africa. Yeye hufanya kazi juu ya maswala ya haki za binadamu, mazingira, exploitation of raw materials, na anavutiwa sana na maswala ambayo yanashuhudia uthabiti ama resilience wa wakaaji wa mkoa huu walioathiriwa na mizozo kwa siku nyingi.

“Niliheshimiwa kueleza hadisi yenye nguvu kama na hii, na kukutana na mwanamke hodari nyuma ya barua hii. Ilikuwa muda bora nilikaa naye Désanges Kabuo na familia yake wakati tulikua tukifanya filamu huko Minova. Sikueleza tu hadisi ya mwanamke aliyefazaishwa na ubakaji ila hadisi ya mwanamke hodari na mapigano yake ya kudumu na ya kujitolea kutoa uhai na matumaini kwa waathirika wa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Hadisi yake Désanges ni yenye nguvu mnoo na iliniomba kupata namna ya pekee ya kuyaeleza. Kwa hiyo, nilitumika naye Mzee Petna Ndaliko, Mwalimu wangu katika image criticism na upigaji picha za haki za kijamii. Alishiriki sana kama mshauri na kwa maoni.

Ninashukuru timu yote nzuri ambayo tulifanya kazi pamoja (Désanges Kabuo, Maitre Amani Kahatwa Mireille, Leslie Thomas, Petna Ndaliko, ART WORKS Projects pia Yole!Africa).

Kazi ya kila mmoja ilikuwa ya muhimu sana kwa kufanikiwa kwa filamu hii.”

— Bernadette Vivuya

 

Produced by
Leslie
THOMAS

Produced by
Désanges
KABUO

Produced by
Amani
KAHATWA

Produced by
Petna
NDALIKO